(Oyaah!! Shem kama shem )
Shem kama shem utatutoa damu
Shem kama shem we Ndio copy ya mama mkwe
Sio kwa dada tu unapendwa na Baba mkwe
Shem juzi kwa kikao kikuu
Mashemeji wote tumekubaliana mwanetu akuchore tattoo
(Oyaah!! Shem kama shem )
Shem kama shem utatutoa damu
Shem ndoa soon tunakuja na posa (kuja na posa )
Fanya urudi home mwana tutamkosa huyu (tutamkosa)
Kwanza Shem wahuni tumemis pishi lako
Sisi sote tupo upande wako
Hakuna wa kurithi kiti chako
(Oyaah!! Shem kama shem )
Shem kama shem utatutoa damu
Oyaa!!! Shemeji la dunia we mke wetu miaka mia (Shem lake )
Me si nakwambia hapo tunao na tumepania
Yeeh! Una nyota kali sana
mwanetu anakutafakari Sana (Shem )
Nakuchana couple yenu itafika mbali sana (Shem)
(Oyaah!! Shem kama shem )
Shem kama shem utatutoa damu